MISS TANZANIA ACHAFULIWA
Na Ushindi ZabronMISS Tanzania 2010, Genevieve Mpangala, amechafuliwa ndani ya mtandao mmoja na watu wanaodaiwa ni wabaya wake, Amani limenasishwa.
Habari zikaenda mbele zaidi kwa watu hao kuweka namba ya simu ya mkononi ya Genevieve wakieleza kuwa kwa anayemtaka awasiliane naye.
Picha hizo ambazo watu hao wanadai ni za Genevieve zinamuonesha akiwa amesimama, lakini zikachomekwa na nyingine za kutengeneza ambazo eti ni miss huyo akiwa mtupu.
Novemba 6, mwaka huu, paparazi wetu alimtwangia simu kinara huyo wa Bongo mwaka 2010 na kumuuliza ukweli wa picha hizo.
“Ninasikitika sana kwa kashfa hii niliyotengenezewa bila mimi kujua, mtu ametumia picha zangu na nyingine za kuungaunga na namba yangu ya simu katika mtandao akidai eti ni mimi najiuza, jambo ambalo si kweli.
“Katika hali ya kawaida jamani miss kama mimi tena niliyewahi kushika taji la juu naweza kuweka picha na namba zangu za simu na kusema natafuta mabwana? Ukiachilia mbali malezi niliyonayo, hata maadili ya Kitanzania hayaruhusu uchafu huo.
“Picha moja niliyosimama nilipigwa na kaka yangu mjini Morogoro ambako tulikwenda kwenye Miss Morogoro na pale ni hotelini nilikofikia,” alisema mrembo huyo.
Baadhi ya mitandao ya kijamii imeingia lawamani ikidaiwa kutumika vibaya na watumiaji wake. Inadaiwa kuna watu wanatengeneza picha chafu za watu maarufu na kudai ni zao halisia kitendo ambacho si cha kweli.



No comments:
Post a Comment